VIPODOZI VYA KUEPUKA KIPINDI CHA UJAUZITO

Kipindi cha ujauzito ni kipindi nyeti sana kwa afya ya mama na mtoto. Mwili wa mama hupata mabadiliko mengi ya kifisiologia.
Moja wa mabadiliko hayo ni kuongezeka kwa uwezo wa kemikali kupenya kwenye ngozi kwenda kwenye damu na hatimaye kwa mtoto.Hivyo vipodozi ambavyo mama hutumia wakati huu vinaweza athiri afya ya mama na mtoto

.Ni muhimu kujua ni vipodozi gani au kemikali gani zilizopo kwenye vipodozi si salama kwa afya ya mama na mtoto kwa kipindi hiki.
Baadhi ya kemikali za kwenye vipodozi ambazo mjamzito anashauriwa kuepukana nazo ni kama zifuatazo
1. Retinoids ( retin A, accutane, retinoic acid)
Kemikali hiyo hupatikana hasa kwenye vipodozi ambavyo hutolewa hospitali (prescription) kutibu chunusi na kupunguza mikunjo ya ngozi. Kemikali hizo si salama kipindi cha ujauzito, hivyo mama mjamzito anashauriwa kuacha kutumia vipodozi vyenye kemikali hizi kwa kipindi chote cha ujauzito

2.Tetracycline.
Kuna vipodozi dawa vya chunusi ambavyo huwa na kemikali hii (antibiotic). Hii pia si salama kipindi cha ujauzito.

3.Hydroquinone
Vipodozi vingi ambavyo hung’arisha au kuchubua ngozi (kuifanya iwe nyeupe) huwa vinakemikali hii. Mama mjamzito anashauriwa kuepukana na vipodozi hivi kipindi cha ujauzito.

4. Formaldehyde
Hii hupatikana sana kwenye vipodozi vya kunyoosha nywele, rangi za kucha na gundi za kubandikia kope. Mama mjamzito achague vipodozi visivyo na hii kemikali kwani huweza athiri utengenezwaji wa mtoto.

5. Toluene
Hii kemikali hupatikana zaidi kwenye rangi za kucha. Mama mjamzito atumie rangi za kucha zisizo na kemikali hii.

6. Ammonia
Hii hupatikana katika rangi za nywele nyinyi. Kemikali hii huweza kuathiri ngozi na mapafu., hivyo ni vyema mama mjamzito akatumia vipodozi visivyo na kemikali hii.
Ni muhimu mama mjamzito kusoma orodha ya viungo ( ingredients) vilivyotumika kutengeneza kipodozi fulani na kujiridhisha kuwa ni salama kabla ya kutumia.
Pia mama huyu anaweza pata ushauri wa kipodozi kipi atumie kwa mtaalam wa madawa au mtoa huduma za afya kwa wajawazito aliyeko karibu nae.

Comments

Popular posts from this blog

Kichefuchefu na Kutapika sana wakati wa ujauzito

TATIZO LA KIFAFA CHA MIMBA (ECLAMPSIA)

JE KULA NANASI WAKATI WA UJAUZITO INA MADHARA?