Posts

Showing posts from May, 2021

Kichefuchefu na Kutapika sana wakati wa ujauzito

Image
Ni hali kali na inayoweza kutokea kwa mama mjamzito inayoambatana na kichefuchefu na kutapika sana au kwa namna nyingine ni kitendo endelevu cha kutapika wakati wa ujauzito kunakosababisha kupoteza uzito zaidi ya asilimia 5 ya uzito wa awali. Huweza kupelekea kupoteza uzito, kuwa na lishe duni na kuharibika kwa usawia wa giligili, na kuharibika usawa wa kemikali mbalimbali mwilini. Tatizo hili huambatana na kiwango kikubwa cha homoni ya HCG ambayo hutolewa kwenye kifuko cha mimba. Ukubwa wa tatizo Hutokea sana kwenye wiki 8 hadi 12 za ujauzito, na dalili hupotea wiki ya ishirini kwa wengi lakini asilimia 10ya wenye tatizo hili. Asilimia 0.3 hadi 2 ya wanawake wanaopata mimba katika mwaka huathiriwa na tatizo hili. Vihatarishi Kuwa na ndugu mwenye tatizo hili kama dada, binti wa mama mwenye tatizo hili huwa kwenye hatari ya kupata tatizo hili. Historia ya tatizo kwenye ujauzito ulipita Mimba mapacha Kuwa na hali ya kijeni inayoitwa triploidy na trisomy Kuwa na ujauzito unaoitwa molar au...

TATIZO LA KONDO LA NYUMA (PLACENTA) KUACHIA KABLA YA MTOTO KUZALIWA (Placenta abruption)

Image
Miongoni mwa dharura zinazoweza kuwatokea baadhi ya wajawazito, ambayo husababisha mama kupoteza damu nyingi, kufa kwa mtoto na hata mama mwenyewe ni Placenta abruptio. Neno Placenta abruptio humaanisha hali ya kujitenga kwa kondo la nyuma (placenta) kutoka sehemu ilipojishikilia kwenye ukuta wa tumbo la uzazi (uterus) kabla hata ya mtoto kuzaliwa. Kondo la nyuma au placenta ni kiungo kinachofanya kazi ya kumlisha mtoto akiwa tumboni kwa mama yake. Katika hali ya kawaida, kondo la nyuma hujitenga na ukuta wa mfuko wa uzazi mara baada ya mtoto kuzaliwa. Hali hii husababishwa na nini? Sababu hasa za hali hii zaweza kuwa ngumu kuzibaini ingawa baadhi ya visababishi hivyo vyaweza kuwa Kuumia eneo la tumbo kunakoweza kusababishwa na ajali za gari, kuangukia tumbo au kupata kipigo kikali Kupoteza kwa kiasi kikubwa cha maji yaliyo katika mfuko wa uzazi (amniotic fluid). Maji haya yanaweza kupotea kwa njia nyingi ikiwemo kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya wakati wake au mara baada ya pacha m...

Jinsi ya Kufanya mtoto ale

Image
Wakati wa kumlisha mtoto haitakiwi kupigana ngumi au kupigizana makele, tumia vidokezo vifuatavyo ili kuzuia malumbano ya kulazimishana kula na na ili mtoto apate mlo kamili. Je mwanao ndo anaanza kula? Au mwanao anapenda kucheza tu kuliko kula? Kama ikifika kipindi cha kumlisha mwanao unakuwa unawaza sana namna ya kupamnana nae usihofu kwani haupo pekee, wazazi wengi huhofu kiwango cha watoto wanachokula au ambacho hawali. Hata hivyo, watoto wengi hupata virutubisho na lishe kwa wingi kwa vyakula wanavyokula ndani ya wiki. Mpaka mtoto ajue chakula anachopenda kula fanya mambo yafuatayo. Bonyeza link hapo chini MAMBO YA KUFANYA ILI MTOTO ALE VYEMA Heshimu hamu ya kula ya mwanao-  Kama mwanao hana njaa, usimlazimishe kula chakula au kitu chochote kile cha kutafuna. Vivyo hivyo usimlazimishe mwanao kufasisha sahani yaani kumaliza chakula chote ulichomuwekea. ukifanya hivyo jambo hili huweza kusababisha mtoto kujilazimsha kula. Kwa kuongezea Mtoto anaweza kupata wasiwasi na kukataa au kuw...

KUFANYA MAZOEZI KIPINDI CHA UJAUZITO JE NI SALAMA?

Image
Kufanya mazoezi ni jambo ambalo binadamu wengi hulifanya mara kwa mara ikiwa ni mpango wa kimaisha au hulifanya mara moja moja. Mazoezi ni kitendo cha kuushughulisha mwili kwa njia mbalimbali. Mazoezi yaliyojipatia umaarufu ni kama kutembea, kukimbia, kushiriki michezo mbalimbali na hata watu hutumia vifaa maalumu vya mazoezi kuishughulisha miili yao. Hivi karibuni vituo vingi tuu vya mazoezi ambavyo vilikuwa maarufu kwenye nchi zilizoendelea vinaanza pia kuonekana barani Afrika. Mazoezi ni mazuri kwa afya ya mwili na akili. Na pia mazoezi yanahusishwa kabisa kisayansi kwenye jedwali la kupata afya bora. Ikiwa ni kawaida kabisa watu wa umri wowote ule kushiriki katika mazoezi, huwa inazua mjadala mara kwa mara ni kwa namna gani wajawazito wafanye mazoezi. Kwanza kabisa je wanaruhusiwa kisayansi kufanya mazoezi? Waandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya DW waliwahi kuyasema haya kuhusu mabadiliko ya mtazamo wa kisayansi kuhusu kufanya mazoezi wakati wa ujauzito Nukuu Miaka 20 iliy...

FAHAMU VYAKULA VINAVYOFAA NA VILE VINAVYOZUILIWA WAKATI WA UJAUZITO

Image
Ni vyakula gani vya kuepuka kutumiwa na wajawazito? Ili mtoto azaliwe akiwa na afya njema pamoja na akili timamu, akiwa tumboni lazima alishwe lishe bora na mlo sahihi. Mwenye jukumu la kutoa lishe bora na sahihi kwa kiumbe kilichomo tumboni ni mama. Anatakiwa kujua aina ya vyakula anavyopaswa kula. Vivyo hivyo, anatakiwa kujua aina ya vyakula vya kuviepuka. Katika makala ya leo, tunaangalia orodha ya vyakula vilivyokatazwa. Mama mja mzito haruhusiwi kuvila vyakula vifuatavyo kwa faida ya kiumbe kilichomo tumboni na kwa faida yake mwenyewe: Nyama mbichi Epuka kula samaki au nyama mbichi au iliyopikwa lakini haikuiva vizuri. Utajiepusha na uwezekano wa kula bakteria na vijidudu vingine hatari kwa afya ya mtoto tumboni. Mjamzito anapokula nyama, anatakiwa kuhakikisha imeiva sawasawa. ‘Soseji” na “Sandwich” Mjamzito haruhusiwi kula ‘soseji’, ‘sandwichi’ za nyama na vyakula vingine vilivyotengenezwa kwa nyama. Inaaminika kuwa nyama zinazoandaliwa kwa ajili ya kutengenezea vyakul...

JE KULA NANASI WAKATI WA UJAUZITO INA MADHARA?

Image
Kumekua na imani na  maneno kwamba mama mjamzito hapaswi kula nanasi wala kunywa juisi ya nanasi kwani ina madhara kwa mama mjamzito.Watu wamekuwa wakiamini kwamba ulaji wa nanais wakati wa ujauzito unaweza kupelekea mimba kuharibika au kujifungua kabla ya wakati. Je swali hili lina ukweli wowote ndani yake? Jambo hili si kweli. Japo ndani ya nanasi kuna kiambata kinachhoitwa BROMELAIN ambacho hutumika kutengenezea dawa ya maumivu na kuvimba (ant inflammatory), dawa hii ikitumika kwa mama mjamzito husababisha mimba kuharibika na hairuhusiwi kutumika wakati wa ujuzito.ila kiwango cha kiambata hiki kilichomo kwenye Nanasi ni kidogo sana.Kipo katika kiwango kidogo mno ambacho hakiwezi kuleta madhara yoyote kwa mama mjamzito. Inahitajika ule mananasi 10 kwa wakati mmoja ndo ufikie kiwango cha Bromelain kinachoweza kuleta madhara kwa ujauzito. Hivyo basi ulaji wa nanasi wakati wa ujauzito hauna madhara bali ni muhimu kwa nanasi lina kiwango kikubwa cha Madini chuma(iron) na folate ambayo ni...

TATIZO LA KONDO LA NYUMA KUMTANGULIA MTOTO(PLACENTA PREVIA)

Image
Placenta previa ni miongoni mwa hali za hatari na dharura inayowapata baadhi ya mama wajawazito ambapo kondo la nyuma hujipachika katika sehemu ya chini ya mfuko wa uzazi, kukua na kisha kufunika sehemu ndogo au kubwa ya njia ya uzazi inayoelekea kwenye shingo ya uzazi na hivyo kuzuia kabisa uwezekano wa mtoto kuzaliwa kwa njia ya kawaida. Chanzo chake ni nini? Wakati wa ujauzito, kondo huongezeka ukubwa na kutanuka kadiri jinsi mfuko wa uzazi unavyotanuka na kukua. Kipindi cha awali cha ujazito, ni jambo la kawaida kwa kondo kuwa maeneo ya chini ya mfuko wa uzazi (low-lying palcenta). Lakini, kadiri mimba inavyokua ndivyo mfuko wa uzazi unavyopaswa pia kulivuta kondo kutoka sehemu za chini na kulipandisha sehemu za juu za kuta zake. Mpaka ifikapo theluthi ya tatu ya ujauzito, kondo linapaswa kuwa karibu kabisa na juu ya mfuko wa uzazi ili kufanya njia ya uzazi kuwa wazi kwa ajili ya kurahisisha utokaji wa mtoto. Hata hivyo, wakati mwingine hayo yote hushindikana kutokea hivyo kusababi...

Kichefuchefu na Kutapika sana wakati wa ujauzito

Image
Ni hali kali na inayoweza kutokea kwa mama mjamzito inayoambatana na kichefuchefu na kutapika sana au kwa namna nyingine ni kitendo endelevu cha kutapika wakati wa ujauzito kunakosababisha kupoteza uzito zaidi ya asilimia 5 ya uzito wa awali. Huweza kupelekea kupoteza uzito, kuwa na lishe duni na kuharibika kwa usawia wa giligili, na kuharibika usawa wa kemikali mbalimbali mwilini. Tatizo hili huambatana na kiwango kikubwa cha homoni ya HCG ambayo hutolewa kwenye kifuko cha mimba. Ukubwa wa tatizo Hutokea sana kwenye wiki 8 hadi 12 za ujauzito, na dalili hupotea wiki ya ishirini kwa wengi lakini asilimia 10ya wenye tatizo hili. Asilimia 0.3 hadi 2 ya wanawake wanaopata mimba katika mwaka huathiriwa na tatizo hili. Vihatarishi Kuwa na ndugu mwenye tatizo hili kama dada, binti wa mama mwenye tatizo hili huwa kwenye hatari ya kupata tatizo hili. Historia ya tatizo kwenye ujauzito ulipita Mimba mapacha Kuwa na hali ya kijeni inayoitwa triploidy na trisomy Kuwa na ujauzito unaoitwa ...

FOLIC ACID KIPINDI CHA UJAUZITO.LINI UNAPASWA KUANZA KUMEZA?

Image
Nimesukumwa kuandika Makala hii na hali iliyopo sasa mama zetu wanameza dawa hizi kutokana na ushauri wanaopewa ili kuongeza na damu na kuwakinga wasizae watoto wenye ulemavu mfano mdomo sungura,mgongo wazi nk. Katika hali ya kusikitisha mama zetu wamekua wakimeza dawa hizi katika njia isiyo sahihi.Nitakuelezea kwa nini. JE NI KATIKA UMRI GANI WA MIMBA UNAPASWA KUANZA KUMEZA FOLIC ACID. Kikawaida viungo vya mwili wa mtoto huwa vinatengenezwa ndani ya miezi mitatu ya mwanzo, Ubongo na uti wa mgongo na mapafu hivi hutengenezwa kati ya siku ya 20 hadi 25. Matatizo katika utengenezwaji wa ubongo na viungo vingine hutokea ndani ya siku 28 za ujauzito.Na kipindi hiki mjamzito anakua bado hajafahamu kama ni mjamzito wengi wao uanza kujigundua baada ya mwezi mmoja.Mama wengi huanza clinic wakiwa na umri wa mimba wakiwa na miez mitatu kuendelea na hapo ndipo wanaanza kupewa folic acid.Kwa hiyo kipindi hiki tayari kama kuna matatizo yamesatokea na folic acid hazimsaidii tena...

UPUNGUFU WA DAMU KIPINDI CHA UJAUZITO (ANAEMIA IN PREGNACY)

Image
Upungufu wa damu (anaemia) hutafsiriwa kama kupungua kwa kiwango cha hemoglobin katika damu damu chini ya kiwango kinachokubalika kiafya. Kiwango cha kawaida cha haemoglobin (Hb) katika mwili wa binadamu ni kati ya gramu 12 mpaka 14 kwa kila mililita ya damu. Hata hivyo shirika la afya duniani (WHO) linatambua kiwango cha mpaka 11gm/mililita kuwa cha kawaida kwa mama mjamzito. Hivyo basi mjamzito mwenye kiwango chochote cha haemoglobin chini ya 11 gm/mililita hutafsiriwa kuwa na upungufu wa damu. Hata hivyo nchi nyingi hasa zinazoendelea hutambua kiwango cha mpaka gramu 10 kwa mililita kuwa ni upungufu wa damu kwa mjamzito.Kwa mjamzito anayehudhuria kliniki kwa mara ya kwanza, upungufu wa damu kipindi cha ujauzito humaanisha kiwango  cha hemoglobin chini ya <11.0 g/dL, na mimba inapofikisha wiki 28 upungufu wa damu hutambuliwa iwapo hemoglobin itashuka na kuwa chini ya 10.5 g/dL. Kwa kuzingatia hilo, mama mjamzito hushauriwa kupima wingi wa damu siku anapohudhuria kliniki kwa mara y...

TATIZO LA KIFAFA CHA MIMBA (ECLAMPSIA)

Image
. Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaohusiana na msukumo mkubwa wa damu (high blood pressure) wakati wa ujauzito pamoja na kuharibika kwa viungo muhimu mwilini kama vile figo na ini. Kwa kawaida ugonjwa huu hutokea baada ya nusu ya kwanza ya ujauzito kuisha (kuanzia wiki ya 20 au miezi mitano ya ujauzito). Ugonjwa huu huweza kuwatokea hata wajawazito ambao hawakuwa na tatizo la msukumo mkubwa wa damu kabla ya ujauzito. Ugonjwa wa kifafa cha mimba unaweza kuleta madhara makubwa kwa mjamzito na mtoto aliye tumboni. Kuharibika kwa viungo muhimu kama figo na ini la mjamzito kunaweza kuwa kwa kiwango kikubwa kichoweza kusababisha mjamzito kupoteza maisha iwapo hatapata huduma ya afya mapema. Vilevile mtoto aliye tumboni anaweza kuathirika kwa kukosa damu ya kutosha toka kwa mama na kushindwa kukua vizuri na iwapo hali hiyo ikiendelea muda mrefu anaweza kufia tumboni. Kutokana na hatari kubwa ya ugonjwa huu kwa wajawazito na watoto walio tumboni, inashauriwa kila mjamzito awe anahudhuria clinic ...

DALILI ZA UJAUZITO

Image
Dalili za ujauzito hutofautiana kati ya mwanamke mmoja  na mwanamke mwingine, ingawa kuchelewa au kukosa hedhi ni dalili moja muhimu sana ya ujauzito. Ni muhimu kuzitambua na kuzifahamu dalili hizi kwa sababu zinaweza kusaidia kujua kama kweli umeshika ujauzito au la  pamoja na kuweza kutofautisha matatizo mengine yanayoshahabiana kwa dalili na  ujauzito. Hebu sasa tuangalie dalili na ishara za ujauzito: Kutokwa damu kidogo ukeni wakati kiumbe kikipandikizwa kwenye mfuko wa uzazi, ingawa siyo wanawake wote hupatwa na dalili hii Kukosa hedhi, hii ni moja ya dalili kubwa ya ujauzito Maumivu kwenye matiti na kuvimba matiti (huweza kutokea kati ya wiki ya 1 hadi ya 2) Uchovu, wanawake wengi huhisi uchovu na  na hali ya kutopenda kufanya lolote. Kupoteza ladha au kuhisi ladha ya chuma mdomoni Kuongezeka kwa hisia ya harufu, kipindi cha ujauzito wanawake wengi huongezeka hisia ya harufu Kichefuchefu na kutapika Maumivu ya kichwa Kizunguzungu Kukojoa mara kwa mara (hasa kati ya wiki 6-8) Kuba...

Madhara ya Unywaji wa Pombe wakati wa Ujauzito

Image
Kati ya mambo ambayo watu wengi hawatilii maanani sana ni unywaji wa pombe wakati wa ujauzito. Nimekuwa nikiwaona akina mama wajawazito wengi wakinywa pombe kwenye sehemu za starehe na sherehe mbalimbali. Hata hivyo si nia ya makala hii kuwazuia kunywa pombe bali kuwapa elimu sahihi juu ya unywaji wa pombe wakati wa ujauzito. Baadhi ya wataalam wanasema unywaji wa wastani wakati wa ujauzito ni kitu ambacho kinaweza kukubalika ingawa wapo baadhi ya wataalamu wengine wanaoamini kuwa unywaji wa hata glasi moja ya mvinyo (wine) kwa wiki huhatarisha afya ya mtoto wako. Hata hivyo haijulikani kwa hakika, ni kiasi gani cha pombe ni salama kwa makuzi sahihi ya mtoto wako tumboni. Wataalamu wengi wanashauri kuacha pombe kabisa wakati wa ujauzito. Pombe inaweza kuleta madhara makubwa kwa mtoto wako bila wewe kuhisi madhara yake. Na yanaweza kuwa madhara ya kudumu ambayo ataishi nayo maisha yake yote. Aidha kuna dhana imejengeka kwa baadhi ya wajawazito kuwa, hawatakiwi kunywa pombe kali kama vod...

KUHARIBIKA KWA MIMBA (Abortion)

Image
Tatizo la mimba kutoka au kutolewa ni jambo ambalo limewakumba kina mama wengi walio katika umri wa kuzaa. Aidha mijadala kuhusu kuhalalishwa au kuendelea kuharamishwa kwa utoaji mimba ni jambo linalochukua nafasi ya mazungumzo ya kila siku katika maisha yetu. Kwa baadhi ya nchi, suala la utoaji mimba ni jambo lililohalallshwa kisheria ingawa kwa nchi kama Tanzania, suala hili halijahalalishwa isipokuwa tu pale panapokuwa na sababu za kitabibu zinazolazimisha kufanya hivyo. Nini maana ya mimba kutoka? Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), utokaji mimba (abortion) hutokea pale ambapo kiumbe (mimba) kilicho chini ya wiki 22 kinapotoka kwa sababu moja ama nyingine, au kinapotolewa kwa njia yeyote ile. Aidha shirika la Afya limekwenda mbali zaidi na kutoa maana nyingine ya utokaji mimba kuwa ni pale mtoto (kiumbe) anapozaliwa akiwa na uzito wa chini ya gram 500. Aidha baadhi ya matabibu hupendelea kutumia neno ‘abortion’ kumaanisha kitendo cha utoaji wa mimba kinachofanyw...