UMUHIMU WA KUACHA NAFASI KABLA YA KUZAA MTOTO MWINGINE (BIRTH SPACING)

Shirika la afya duniani (WHO) linashauri wazazi kukaa angalau miaka miwili kabla ya kupanga kupata mtoto mwingine.
Wazazi wengi wa sasa wamekuwa wakichagua kufululiza kuzaa ili waweze kumaliza uzazi haraka, Ukweli ni kwamba kufanya hivi husababisha madhara kwa mama na mtoto mtarajiwa.

FAIDA ZA KUACHA NAFASI NI ZIPI?

-Huandaa mwili wa mama kuwa na virutubisho vya kutosha kwa ajili ya mtoto mtarajiwa na vya kutosha kumuacha mama katika afya nzuri wakati wa uzazi na baada ya kujifungua.
-Huruhusu wazazi wawe na nguvu za kulea mtoto wa kwanza vizuri.

Madhara ya kutoacha nafasi ni yapi?

-Kuzaa kabla ya wiki ya 37 na hivyo kupata mtoto mwenye uzito mdogo.
-Kupata shida wakati wa kujifungua na kuweza kupelekea kuchanika kwa mfuko wa uzazi.
-Huweza kupelekea kifo cha mtoto au mzazi kwa sababu ya kutokuwa na virutubisho vinavyotosha.
-Huweza kupelekea kutokwa na damu ukeni katika miezi mitatu ya mwisho.
-Huweza kupelekea mama kupata sonona ya uzazi.
-Kwa mtoto aliyezaliwa kwanza, kuachwa kunyonyeshwa kwa ajili ya kuweka virutubisho kwa mtoto mtarajiwa humkosesha maziwa ya mama ambayo ni muhimu sana katika miaka miwili ya kwanza.

MUHIMU:-
-Kwa wakina mama waliopoteza watoto (miscarriage) au mimba kutoka, wanatakiwa kusubiri angalau miezi 6 kabla ya kujipanga kwa mtoto mwingine kupunguza madhara yaliyotajwa hapo juu.
-Wazazi wanatakiwa kujadili njia nzuri ya uzazi wa mpango ambayo itaweza kuwasaidia kwenye miaka miwili hii. Iwapo watapata shida kujua wafanye nini, watembelee hospitali ili waweze kuonana na daktari atakaewasaidia

Comments

Popular posts from this blog

Kichefuchefu na Kutapika sana wakati wa ujauzito

TATIZO LA KIFAFA CHA MIMBA (ECLAMPSIA)

JE KULA NANASI WAKATI WA UJAUZITO INA MADHARA?