JINSI GANI MAMA MWENYE VVU ANAWEZA KUMKINGA MTOTO ALIE TUMBONI ASIZALIWE NA MAAMBUKIZI

Je, watu walioambukizwa VVU wanaweza kupata au kuzaa watoto ambao hawana virusi?
Ndio.
•  Hii ni mojawapo ya faida nyingi za matibabu ya VVU (ART).
•  Unaweza kupata watoto ukiwa umeadhirika na VVU.
•  Tafadhali zungumza na daktari wako ikiwa umeamua kuwa mjamzito.
•   watu wanaoishi na VVU wanapaswa kupokea huduma na msaada sawa na watu wasio na VVU.

•  ART inamlinda mshiriki wakati wa utungaji wa mimba ikiwa mwenziwe ana VVU
•  ART inamlinda mtoto dhidi ya VVU wakati wa ujauzito na wakati wa kuzaliwa
 MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA ILI KUMKINGA MTOTO ALIE TUMBONI ASIPATE MAAMBUKIZI
 

Matumizi sahihi ya ART kama ashauriwavyo na wataalamu wa afya. dawa hizi hupunguza idadi ya virusi hivyo huepusha maambukizi kwa mtoto wakati wa ujauzito na kujifungua.

Mama anapaswa kuzingatia usafi binafsi ili kuzuia maambukizo ya vimelea vya magonjwa. baadhi ya magonjwa huharibu plasenta hivyo kupelekea urahisi wa virusi kupita toka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito

mama anapaswa kula mlo kamili na wenye lishe bora wakati wa ujauzito. itamuwezesha mama kuongeza kinga dhidi ya magonjwa nyemelezi.

Mama anapaswa kuandaa mazingira salama ya kujifungua, hii ni pamoja na kuwahi kituo cha afya mara amapoona dalili za mwanzo za kujifungua. humwepusha mama kupata matatizo wakati wa kujifungua na pia mtoto atapata dawa za kujikinga na maambukizi mara tu baada ya kuzaliwa

Ni wakati upi mtoto yupo hatarini kupata maambukizo ya VVU kutoka kwa mama?

  •  wakati wa ujauzito, hasa mama anapopata maambukizo mapya kwani idadi ya virusi (viral load) huongezeka 
  • wakati wa kujifungua kama mtoto atapatwa na michubuko itakayo ruhusu virusi kutoka kwenye damu ya mama kupenya kwa mtoto 
  • wakati wa unyonyesha endapo mama atazidisha kumnyonyesha mtoto baada ya miezi sita au kumpa vyakula vingine kabla ya miezi sita.

Comments

Popular posts from this blog

Kichefuchefu na Kutapika sana wakati wa ujauzito

TATIZO LA KIFAFA CHA MIMBA (ECLAMPSIA)

JE KULA NANASI WAKATI WA UJAUZITO INA MADHARA?