ATHARI ZA PUMU KATIKA UJAUZITO
- Get link
- X
- Other Apps
Pumu ni ugonjwa ambao huathiri sehemu ya kupitisha hewa (bronchioles) kwenda kwenye mapafu. Sehemu hiyo huvimba na kuzalisha ute mzito (mucus), hivyo huzuia hewa ya kutosha kuingia mapafuni.Kuna makundi mawili ya pumu; Pumu ya ghafla(Acute athma) na Pumu sugu (Chronic athma).
Katika pumu ya ghafla, mgonjwa huwa na hali ya kawaida tu, ila pumu inapo amka hupata matatizo ya kupumua na kifua kubana. Kwa upande wa pili, Pumu sugu huambatana na wembamba katika njia au sehemu za kupitishia hewa kwenda mapafuni na mgonjwa hupata matatizo ya kupumua na kifua kubana mara kwa mara.
Ugonjwa wa pumu husababishwa na mambo mengi kama vile; Vinasaba au kurithi, Uvutaji wa sigara au tumbaku wakati wa ujauzito husababisha ugonjwa wa pumu kwa mtoto atakayezaliwa,Vyanzo vya mzio(allergens) kama vile vumbi na baadhi ya vyakula, moshi na harufu kali kama vile perfumes, kemikali katika maeneo ya kazi kama vile viwandani na magonjwa kwenye mfumo wa upumuaji yanayosababishwa na virusi au bacteria.
Dalili za ugonjwa wa pumu ni ; Kuishiwa pumzi (shortness of breath), kutoa sauti za miluzi wakati wa kupumua(wheezing), kukohoa sana hasa asubuhi na usiku na kifua kubana.
ATHARI ZA PUMU KATIKA UJAUZITO
- Mara nyingi pumu ya ghafla huwa haina madhara sana kwa mjamzito, ila inapokuwa sugu na dalili zake kujitokeza mara kwa mara kama vile kukosa pumzi na kifua kubana husababisha mtoto kukosa hewa safi ya oksijeni maana mtoto hutegemea hewa ya mama awapo tumboni. ukosefu wa hewa huu husababisha mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mdogo kupita kiasi.
- Pumu husababisha homa kali ya asubuhi (severe morning sickness)
- Husababisha matatizo kwenye kondo la uzazi au placenta na hivyo huchangia sana katika matatizo ya namna ya kujifungua muda unapofika.
- Pumu husababisha shinikizo la damu kupanda kwa mjamzito, shinikizo kubwa la damu husababisha matatizo mengine mengi kama vile magonjwa ya moyo endapo halitatibiwa.
- Pumu husababisha damu kuvuja Ukeni wakati wa uajuzito, jambo linaloweza kusababisha upungufu wa damu.
je!, dawa za pumu ninazotumia hazitaleta madhara kwa mwanangu? mara nyingi dawa hizi huenda mapafuni moja kwa moja ili kusaidia kuondoa dalili mbaya za pumu, hivyo basi mjamzito mwenye pumu aendelee kutumia dawa za pumu kwa kufuata maelekezo ya daktari kwa umakini mkubwa sana, kwa kufanya hivyo ujauzito wake utakuwa na afya tele kwa mtoto.
NINI KIFANYIKE ILI KUEPUKANA NA MADHARA YA ATHMA KATIKA UJAUZITO WANGU?
- Fahamu visababishi (triggers) vya pumu kwako kama vile vumbi, moshi wa sigara, hali ya hewa kama vile baridi, viepuke kabisa.
- Fuata masharti ya Daktari na tembelea vituo vya tiba mara kwa mara ili uepukane na dalili mbaya za pumu.
- Fanya mazoezi kwa uangalifu mkubwa kwa sababu mazoezi huweza kuleta dalili mbaya za pumu, fuata ushauri wa dakatari juu ya namna ya kufanya mazoezi kwa uzuri zaidi.
- Fahamu dalili hatarishi za pumu; una matatizo ya kupumua, mtoto hachezi tumboni au dawa zako zimeacha kufanya kazi, hivyo tafuta msaada kwa daktari.
- Get link
- X
- Other Apps

Comments
Post a Comment